Cytonn Blog

Hongera Cytonn

Joseph Muriithi Nov 24, 2016 13:11 0 comment(s)

Ya mgambo ishalia, Lipo la mno tegea,

Nijongee karibia, Uhondo nakumwagia,

Wekezaji pulikia, Sije kalipuuzia,

Hongera kwenyu Cytonn, Ahadi mwatimizia,

 

Amara Mulizindua, Kareni ikaduwaa ,

Asilimia kwa mia, Yote kesha wauzia

Wekezaji wavunia, na kivulini hulia,

Hongera kwenyu Cytonn, Ahadi mwatimizia,

 

Situ nayo mwajengea, Kwa kina ufasaha pia,

Vijumba vilo ng’aria, vya dhamani dhamania,

Kwa ubali vya vutia, Sote twaikaribia,

Hongera kwenyu Cytonn, Ahadi mwatimizia,

 

Aluma nawelezea, kitazama waduwaa,

Kinywa chako wapanua, neno sijekatokea,

Enyi mloijengea, Kiti twamuondokea,

Hongera kwenyu Cytonn, Ahadi mwatimizia,

 

Ewe Dande Lizi pia, Sifa nawamiminia,

Huko juu mwapepea, taji ninawavishia,

Uwekezaji bandia, Kisogo ninaupea,

Hongera kwenyu Cytonn, Ahadi mwatimizia.


Mtunzi:   Catherine N. Murigi
               PR & Communication Intern
( 0 ) Comment(s)


Please login to post comment
© 2017 Cytonn Investments Management Ltd